Wachungaji kutoka Mwanza walitembelea studio ya Radio Sauti ya Injili na kuuliza swali hilo:
Jibu:- Kwanza inatakiwa uwe na uwanja juu ya mlima,Kwasababu Mawimbi ya masafa ya FM yanatembea umbali unaoweza kuona nani eneo dogo tu. Hayawezi kupita mlima mwingine maanake nyuma ya ule mlima mwingine wasikilisaji watakuwa kivulini na hawataweza kusikia chochote.
Halafu tunahitaji Umeme wa Tanesco kule Juu ya Mlima:
Pia tunahitaji mitambo nakujenga Banda juu ya mlima kufunga mitambo hiyo, kwa ile mitambo a watts 250 tunatumia banda ndogo inatosha. Kama unapenda kusikika eneo kubwa zaidi na mitambo yake ni zaidi ya watts 1000 unahitaji nyumba kubwa zaidi.
Kariabu ya ile nyumba ndogo tunahitaji mnara na antenna zake. Aina gani ya antenna inategemea na eneo unalopenda isikiki..
Ndani ya ile nyumba ndogo tunaweka ile mitambo (transmitter) na vyombo kuunganisha na studio (Link).
Lakini muhimu sana ni kupata kibali cha serekali, na kupata liseni ya ile mitambo kutoka TCRA. Bila Liseni huwezi kupata Frequency kuenda hewani.Kituo cha Radio Sauti ya Injili bado wanahitaji msaada kupata hivyo vyote ili kuendelea kuwa hewani.
Haya yote yanapatikana namna gani?
Mahali pengine Askofu wa Dayosisi ameomba donors mbalimbali kusaidia gharamaza kununua mitambo na antennas. Mnara ya antenna imetengenezwa hapa Tanzania.
Marafiki wamesaidia kupata uwanja juu ya mlima na wanasaidia hata ulinzi wa mahali pale pia.