ELCT
Press Release
(English) Salamu kuhusu uchomaji moto makanisa Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) tarehe 18 Oktoba walikwenda Mbagala, jijini Dar es Salaam kuwafariji washarika kutokana na tukio la kanisa lao kuchomwa moto na wanaharakati wa dini ya Kiislamu hivi karibuni. Maaskofu hao wa KKKT walitoa ujumbe ufuatao:
Wapendwa
Katika Bwana, Neema na Iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba na Bwana wetu Yesu Kristo, Amina. Sisi maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), tumepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za matukio ya uchomaji wa makanisa katika eneo hili la Mbagala. Tumekuwa katika mkutano wetu wa Mwaka wa Lutheran Mission Cooperation (LMC) huko Moshi pamoja na vyama vyote vya Kimissioni vya Ulaya na Marekani. Tumelazimika kukatisha mkutano huo ili kufika hapa Mbagala. Tumekuja kwa madhumuni makubwa matatu:
Katika
ujio huu wa maaskofu hapa Mbagala, hatukuja hapa kufanya haya yafuatayo:
Wapendwa wana KKKT na watukuka sana, wana na mabinti wa Tanzania ya Julius Kambarage Nyerere; kilichotokea Mbagala katika wiki ya kuadhimisha siku ya Baba wa Taifa, ni kebehi si kwa Baba wa Taifa bali ni kebehi kwetu sisi wenyewe tunaokalia kiti alichokalia Baba wa Taifa. Yeye amelala baada ya kazi njema. Apumzike kwa amani na tunu zake zifufuke katika majivu haya yaliyotokana na kuchomwa kwa amani na mshikamano wa Tanzania aliyoijenga. Kilichotokea Mbagala ni mateso ya kimbari, yaani mateso ya Kanisa (Persecution). Mateso haya ni matokeo ya mbegu ya magugu iliyopandwa katika bustani njema na sasa magugu hayo yanazaa matunda machungu. Dalili za mateso ya kimbari kama ilivyo kwa mateso ya kanisa; zilianza kitambo na hazikushughulikiwa na waliomrithi Baba wa Taifa. Dalili hizo ni kama hizi zifuatazo:
Wapendwa wana KKKT na Wapendwa watanzania wote. Hata kama wanaofanya mambo haya ya kusikitisha wametunukiwa hadhi ya kuitwa kuwa ni wana harakati, tofauti na wanaharakati wanaotambuliwa na watanzania walio wengi, tunawiwa kuonya kwa uvumilivu wote kuwa uana harakati wao usitumike kuvunja nchi na sheria za nchi. Tanzania yenye amani na mshikamano ni tunda la dini zote, makabila yote, itikadi zote za vyama, rangi zote na hali zote za kiuchumi. Hata wasio na dini wanachangia amani ya nchi hii. Kwa macho na masikio yetu, tumeendelea kushuhudia vitendo vya uchomaji makanisa huko Zanzibar, Mwanza, Mdaula, Mto wa Mbu, Tunduru, Rufiji, Kigoma na sasa Mbagala. Wakati wote uvumilivu wa wakristo huenda umetafsiriwa kuwa ni unyonge na woga. Ikumbukwe kuwa hata wanyonge na waoga, hufika wakati wakasema sasa basi pale wanapodhalilishwa kupita kiasi. Hatuombei wakristo wafikishwe hapo. Tumeshuhudia wizara zetu zikivamiwa mchana kweupe na kushinikiza kuachiwa kwa watuhumiwa wa uhalifu; tumeshuhudia vituo vya polisi vikichomwa moto; mahakama zikilazimishwa kufunga shughuli zake, misikiti ikitekwa, uhai wa viongozi wa dini ukitishiwa hadharani na viongozi wastaafu wakizabwa vibao hadharani kwa sababu ya zinazoitwa harakati za kidini. Tumefikia kuhoji, watu hawa wavamie nini ndipo hatua zichukuliwe? Wachome nini ndipo viongozi wenye dhamana ya kulinda mali na uhai washtuke? Wamwue nani ndipo iaminike kuwa watu hawa ni tishio kwa usalama wa taifa letu? Sisi tulioitwa kwa njia ya nadhiri na viapo vitakatifu, tunawasihi sana waumini wa dini zetu na watanzania kwa ujumla, wenye wajibu wa kututii na wasiolazimika kututii, kuzingatia kuwa Mwenyezi Mungu analipenda taifa hili na watu wake. Kamwe hawezi kuliacha liangamie. Kwa Wakristo wote, huu ni wakati wa kuendelea kufunga na kuomba kwa ajili ya amani ya taifa hili. Mkristo wa kweli ni yule aliye tayari kuteswa kwa ajili ya Kristo na kanisa. Wakristo hatuko tayari kuua, kutesa, kulipiza kisasi ili kumtetea Kristo. Mungu wetu hatetewi kwa kuua wengine na kuchoma madhabahu ya dini nyingine. Katika mateso haya, kanisa litaimarika zaidi; na katika majivu haya ya Mbagala, Tanzania mpya itazaliwa na ukombozi wa kweli utapatikana. Tunawataka wakristo wote kusamehe na kuendelea kuwa raia wema. Kushiriki kikamilifu katika kuleta mabadiliko ya kweli kwa kupitia njia sahihi zilizowekwa. Wakati wengine wanaweka mikakati ya kuchoma madhabahu, wakristo tuweke mikakati ya kuomba na kushiriki vema katika haki zetu za uraia. Pamoja na kuwa wapole kama njiwa, imetupasa pia kuwa na busara kama nyoka (Mathayo 10:16). Daima tukumbuke kuwa, KUSHINDANA KWETU SISI SI JUU YA DAMU NA NYAMA BALI NI JUU YA FALME NA MAMLAKA, JUU YA WAKUU WA GIZA HILI, JUU YA MAJESHI YA PEPO WABAYA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO (Waefeso 6: 12). Ni sisi
Maaskofu wenu kwa Neema ya Mungu,
Issued
by the: ================================================== |
|
For more information contact: Elizabeth
Lobulu |