ELCT
Press Release Date:
July 14, 2015 |
|
Mkutano
Mkuu ni Makumira tena Katibu Mkuu wa KKKT, Bw. Brighton Killewa, amesema hivi karibuni kwamba Mkutano huo Mkuu utaongozwa na Neno Kuu: Jitahidi kuuhifadhi umoja wa roho katika kifungo cha amani (Efeso 4: 3). Mkutano Mkuu hufanyika kila baada ya miaka minne na lengo ni kupokea, kujadili taarifa mbalimbali na kuweka malengo na mwelekeo wa miaka ijayo. Mkutano Mkuu pia huchagua viongozi mbalimbali kama Mkuu wa KKKT, Mwandishi na Wajumbe wa Halmashauri na Kamati mbalimbali za Kanisa. Somo la Biblia litaongozwa na Askofu Mstaafu Dkt. Hance Mwakabana Na Somo hilo litaanza kutolewa siku ya ufunguzi na kuendelea kwa siku zote za Mkutano. Pia wajumbe watashiriki warsha ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa na kujadiliwa. Mada zitaongozwa na kauli mbiu isemayo: umoja na utambulisho wetu. ================================================== |
|
For more information contact: Elizabeth
Lobulu |