ELCT
to assists victims of the earthquake in Kagera
The Presiding
Bishop of the Evangelical Lutheran Church in Tanzania (ELCT) closed
the Pastors Conference held in Dodoma 24 to 29 September with
a call to its members demonstrate their love for one another by
making contribution for victims of an earthquake that struck Kagera
recently.
He said this
when he handed over Sh. 240 million/= donation to assist victims
of the earthquake to Bishop Dr. Abednego Keshomshahara of ELCT
North-western Diocese in Kagera region. The money was contributed
by some of the ELCT Bishops and some of the ELCT partners abroad.
The offering at the opening service of the conference was also
directed to assist the earthquake victims.
He explained
that love should be shared by helping those in need at a time
such as the earthquake in Kagera. He urged dioceses to collect
donations from the members of the church for the victims.
He pointed
out that donations will be given to all victims in Kagera Region
- including North-western Diocese and Karagwe Diocese - without
any kind of discrimination on the basis or religion, gender, political
affiliation.
With a 5.7
magnitude that struck 22km northeast of Nsunga, Kagera region
on Sunday night 10 September 2016 sending shock waves in the Lake
Zone area in Tanzania and the neighbouring country of Uganda and
Kenya. It claimed the lives of 19 people and 253 injured in Tanzania.
As soon as
the earthquake struck, he said ELCT through its planning Department,
ACT Alliance, the World Service of the Lutheran World Federation
(LWF) and the Diaconia arm of ELCT the Tanganyika Refugee
Services (TCRS) dispatched a team to assess the situation and
delivered some blankets, tents, bedding and schools uniforms.
More of the material -including blankets, school supplies and
clothing have been given to the leadership of the two dioceses.
The meeting
was attended by at least 1,500 pastors from the ELCT dioceses,
institutions and mission areas. The theme of the Conference was:
The 500 years of Reformation: Our witness was addressed
by Bishop Dr. Keshomshahara. Other presentations were on: The
Pastor and Christian Education, presented by Rev. Dr. Emmanuel
Kileo; The Church and Revival, by Rev. Dr. Faith Lugazia;
Pastoral Counselling, by Rev. Dr. Angela Olotu and
The Pastor and worship, by Rev. Dr. Msafiri Mbilu.
The presentations
are available in Swahili at the links below:
|
Kanisa
kusaidia walipatwa na tetemeko Kagera
Mkuu wa Kanisa
la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) alifunga mkutano wa Wachungaji
uliofanyika Dodoma 24 to 29 Septemba kwa wito kwa wanachama wake
kuonesha upendo kwa vitendo kwa kuchangia ili kusaidia waliopatwa
na tetemeko mkoani Kagera hivi karibuni.
Alisema hayo
alipokuwa akimkabidhi mchango wa Sh. 240 million/= kwa Askofu
Dkt. Abednego Keshomshahara wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi
iliyopo Mkoa wa Kagera. Fedha hizo zilichangwa na wajumbe wa Halmashauri
Kuu ya KKKT na baadhi ya washirika wa KKKT walio nje ya nchi.
Pia sadaka iliyopatikana wakati wa Ibada ya Ufunguzi wa Mkutano
huo wa Wachungaji utapelekwa kuwasaidia waathirika wa tetemeko.
Alisema upendo
lazima uoneshwe kwa matendo kwa kugawana na kuwasaidia wengine
wenye uhitaji kama ilivyo kwa wale walioathirika na tetemeko Kagera.
Alihimiza Dayosisi zikusanye michango toka kwa washarika endapo
bado hawajachanga kwa ajili ya waathirika hao.
Aidha alisema
michango yote itakayotolewa itakuwa ni kwa ajili ya waathirika
wote Mkoani Kagera ikiwemo Dayosisi ya Kaskazini Magharibi
na Dayosisi ya Karagwe bila kubagua dini, jinsi au chama
chake cha kisiasa.
Tetemeko lililokuwa
na kipimo cha 5.7 lilikumba eneo kilomita 22km kaskazini mashariki
ya Nsunga, Mkoani Kagera usiku wa kuamkia 10 Septemba 2016 na
athari zake kufika eneo la ukanda wa Ziwa nchini Tanzania hadi
nchi jirani za Kenya na Uganda. Watu 19 walikufa na wengine 253
walijeruhiwa nchini Tanzania.
Mara baada
ya tetemeko hilo kutokea, Askofu alisema KKKT kupitia Idara yake
ya Mipango, Shirika la Maafa la Kimataifa Act-Alliance Tawi la
Tanzania, Shirika la World Service la Fungamano la Makanisa ya
Kilutheri Duniani (Geneva) na Mkono wa Diakonia wa KKKT TCRS (the
Tanganyika Refugee Services lilituma timu kwenda kufanya tathmini
ya awali na kupeleka misaada michache ya haraka kama mablanketi,
maturubali, matandiko na unifomu za shule. Baada ya hapo vifaa
vingi zaidi bedding and schools uniforms. Vifaa zaidi kama mabelo
ya mablanketi, maboksi ya vifaa vya shule na mabelo ya nguo zilipelekwa
baadaye ili kukabidhiwa kwa menejimenti ya dayosisi hizo mbili
wazigawe.
Mkutano wa
Wachungaji wa KKKT ulihudhuriwa na wachungaji 1,500 kutoka Dayosisi
za KKKT zilizopo nchi nzima, vituo na maeneo ya misioni ya KKKT.
Neno Kuu la
Mkutano lilikuwa Miaka 500 ya Matengenezo: Ushuhuda wetu
ambapo Askofu Dkt. Keshomshahara alilifundisha. Mada juu ya: Mchungaji
na Elimu ya Kikristo, ilitolewa na Mchg. Dkt. Emmanuel Kileo;
Kanisa na Uamsho, iliyotolewa na Mchg. Dkt. Faith
Lugazia; Ushauri wa Kichungaji, iliyotolewa na Mchg.
Dkt. Angela Olotu na Ibada na Umoja wa Kanisa iliyotolewa
na Mchg. Dkt. Msafiri Mbilu.
Unaweza kupata
mada hizo kwa PDF format kama ifuatavyo:
|