Askofu
Mkuu Musa Filibus awa Rais wa FMKD
Na Elizabeth Lobulu --- Windhoek, Namibia
Askofu
Mkuu wa Kanisa la Kikristo la Nigeria (LCCN), Dkt. Musa Panti Filibus,
amekuwa Rais wa Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani (FMKD) alipoingizwa
kazini katika ibada ya kufunga Mkutano Mkuu wa 12 wa jumuiya hiyo uliofanyika
Windhoek, Namibia tarehe 10 - 17 Mei 2017.
Mkutano huo uliohudhuriwa na watu 800 ulikuwa na kauli mbiu: “Tumeokolewa
kwa neema ya Mungu”. Na wajumbe walipata nafasi ya kusikiliza na
kujadili mada ndogo tatu: “Wokovu si wa kuuzwa”; “Binadamu
si wa kuuzwa” na “Uumbaji si wa kuuzwa”.
Rais mpya
wa FMwa KD Askofu Mkuu Dkt. Filibus Musa akiwa na Askofu Younan Munib
anayeondoka.
Mkutano
huo ulikuwa wa kipekee kwa kuwa pamoja na mambo mengine ulikuwa na sherehe
ya kukumbuka miaka 500 ya matengenezo ya kanisa kimataifa wakati wa
Ibada ya Meza ya Bwana iliyofanyika Uwanja wa Taifa wa Sam Nujoma Windhoek
tarehe 14 Mei 2017.
Mkutano huo uliokuwa na kauli mbiu: ‘Tunaokolewa kwa Neema ya Mungu’,
pamoja na mambo mengine, ulipokea na kujadili hotuba ya Rais anayeondoka
Dkt. Younan; Ripoti ya Katibu Mkuu wa Fungamano, Mch. Dkt. Martin Junge;
mada mbalimbali na kufanya uchaguzi wa Rais na wajumbe wa Halmashauri
Kuu.
Japo alianzia ngazi ya chini eneo la Mayo-Belwa, Askofu Mkuu Musa Panti
Filibus, alichukua mafunzo ya ualimu daraja la pili na hatimaye kufundisha
katika shule za serikali eneo la Mayo-Belwa.
Askofu Mkuu Filibus baadaye alijiunga na Chuo cha Theolojia Kaskazini
mwa Nigeria (TCNN) na kufuzu Shahada ya Mafunzo ya Dini (Bachelors of
Divinity Degree) mwaka 1992. Aliajiriwa kufundisha katika Seminari ya
Ndogo ya Kilutheri Bronnum iliyoko Mbamba Yola, Jimbo la Adamawa kuanzia
1993.
Dkt. Musa alibarikiwa kuwa mchungaji mwaka 1994 kisha akaenda Marekani
kusoma katika Chuo Kikuu cha Kilutheri Minnesota na kupata Shahada ya
Udakatari katika masuala Theolojia na Unasihi Kichungaji.
Alipomaliza mashomo yake alirudi kufundisha katika shule alikotoka ambapo
aliteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo hicho hadi mwaka 2002 alipopokea wito kufanya
kazi FMKD kama Katibu wa Afrika katika Idara ya Misioni na Maendeo Oktoba
2010. Aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara hiyo 2010 hadi Julai 2013.
Askofu Mkuu Musa Panti Filibus aliteuliwa na Kanisa lake kuongoza Dayosisi
ya Mayo Belwa iliyoko kusini Magharibi mwa Nigeria na aliwekwa wakfu
na kuingizwa kazini Oktoba 2013. Alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Makanisa ya Kilutheri Nigeria ndipo Novemba mwaka jana
akachaguliwa kuwaAskofu Mkuu LCCN.
Februari 2017 Makanisa toka Bara la Afrika yalimteua Askofu Mkuu Filibus
kuwa mgombea wa nafasi ya Rais wa Fungamano.
Askofu Musa anachukua nafasi ya Askofu Dkt. Munib Younan wa Kanisa la
Jordan na Nchi Takatifu aliyemaliza kipindi chake 17 Mei 2017.