Martin
Junge Karibu Tanzania
Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) limemwalika Katibu Mkuu
wa Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani (FMKD), Mchg. Dkt.
Martin Junge, kufanya ziara ya kichungaji ya siku nne nchini.
Taarifa iliyotolewa
leo na Katibu Mkuu wa KKKT, Bw. Brighton Killewa, imesema Mchg.
Dkt. Junge atatoa mada kuu kuhusu: Kujenga Jamii na Umoja
wa Kanisa kwenye faragha ya viongozi wa KKKT itakayofayika
Wilayani Karatu kuanzia tarehe 20 hadi 22 Februari 2019.
Baada ya mazungumzo
na uongozi wa Kanisa atatembelea Dayosisi ya Kaskazini kwa siku
nzima ya tarehe 24 Februari 2019 ambapo ataanza kwa kushiriki
na kuhubiri katika Ibada ya Jumapili Usharika wa Gezaulole Wilayani
Hai na kutembelea baadhi ya vituo vya Dayosisi vilivyoko Wilaya
ya Hai, Kilimanjaro.
Katibu Mkuu
huyo wa FMKD atawasili Tanzania tarehe 20 Februari 2019 na anatarajiwa
kurudi Geneva, Uswisi tarehe 24.
Bw. Killewa
alisema faragha hiyo ya viongozi itahudhuriwa na watu 41 wakiwemo
maaskaofu wa KKKT. Mada mbalimbali zitatolewa na kujadiliwa wakati
wa warsha iliyoandaliwa kwenye faragha hiyo.
|
ELCT
welcomes Martin Junge
The Evangelical
Lutheran Church in Tanzania (ELCT) has invited the General Secretary
of the Lutheran World Federation, Rev. Dr. Martin Jungefor a four-day
pastoral visit to Tanzania.
A statement
issued today by the ELCT Secretary General , Mr. Brighton Killewa,
said that Dr. Junge will deliver a keynote address on: Communion
Building and Church Unity during ELCT Church leaders retreat
due to take place 20 22 February 2019.
Among other
things, after carrying out discussions with the ELCT leadership,
he will pay a one-day visit to Northern Diocese on 24 February
2019 starting with delivering of a sermon at a Sunday Worship
Service at Gezaulole Lutheran Parish (Hai District) as well as
tour some institutions run by the diocese in Hai District, Kilimanjaro
Region.
The LWF General
Secretary arrives in Tanzania on 20th February and is expected
to return to Geneva, Switzerland on the 24th February.
Mr Killewa
said 41 people will attend the leadership retreat, including ELCT
bishops. A number of papers will be presented and discussed during
a workshop as part of the retreat.
|